Mark 4:10-12

10 aAlipokuwa peke yake, watu waliokuwepo naye pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili wakamuuliza kuhusu mifano yake. 11 bNaye akawaambia, “Ninyi mmepewa kujua siri ya Ufalme wa Mungu. Lakini kwa wale walioko nje, kila kitu husemwa kwao kwa mifano, 12 cili, “ ‘daima waone lakini wasitambue,
daima wasikie lakini wasielewe;
wasije wakageuka, wakatubu na kusamehewa!’ ”

Isa Afafanua Maana Ya Mfano Wa Mbegu

(Mathayo 13:18-23; Luka 8:11-15)

Copyright information for SwhKC